Mfumo wa mauzo kwa maduka ya Tanzania

Uza haraka. Jua stoo yako. Dai kila deni.

PixelPOS inaendesha kaunta ya maduka, wauzaji wa jumla, famasia na maduka ya vifaa: risiti kwa sekunde, stoo inayolingana, madeni ya wateja wanaolipa baadaye, na faida ya leo kabla hujafunga.

TZS 250,000 kwa mwaka 7 siku za kujaribu bure Hakuna kadi Kiswahili na Kiingereza
Skrini ya mauzo ya PixelPOS yenye bidhaa nne kwenye kikapu na orodha ya bidhaa
Madeni kwenye simu: pesa inayodaiwa na yaliyochelewa

Kwa ajili ya

Maduka ya rejareja Wauzaji wa jumla Famasia Maduka ya vifaa vya ujenzi Maduka ya nguo Saluni Migahawa Vifaa vya elektroniki
Madeni

Kila deni limeandikwa, na linadaiwa

Andika anachochukua mteja kwa mkopo, au deni la duka kwa msambazaji. Pokea malipo kidogo kidogo na uone mara moja nani amechelewa.

  • Madeni ya kupokea na ya kulipa, kila moja na jumla yake
  • Madeni yaliyochelewa yanaonekana kwa tarehe uliyoweka
  • Mkumbushe mteja kwa WhatsApp kwa kubofya mara moja, na kiasi kimeshaandikwa
Ukurasa wa Madeni wenye kiasi kinachodaiwa, madeni yaliyochelewa na salio la kila mteja

Mauzo ya haraka

Soma barcode, chapisha risiti, shikilia mauzo mteja mwingine akilipa.

Stoo inayolingana

Manunuzi, uhamisho na marekebisho, na tahadhari kabla bidhaa haijaisha.

Faida kila siku

Ulichouza, kilichogharimu na ulichopata, kwenye ripoti unazoweza kupakua.

Akaunti kwa kila mfanyakazi

Wewe unaamua kila mtu anaona nini na anafanya nini, hadi nani anaweza kupokea malipo.

SMS kwa wateja wako

Tuma ofa na makumbusho kwa wateja wote kwa mara moja, kwa jina la duka lako.

Siri na nakala salama

Kila duka lina database yake, iliyotengwa na maduka mengine yote.

Vifurushi

Bei moja kwa mwaka
Ongeza vifaa ukivihitaji

Kila kifurushi ni PixelPOS kamili. Tofauti ni vifaa unavyoweka kaunta.

PixelPOS

Programu kwa mwaka mzima

TZS 250,000
kwa mwaka
  • PixelPOS kwa miezi 12: mauzo, stoo, madeni, ripoti
  • Inafanya kazi kwenye simu, tablet au kompyuta uliyonayo
  • Jaribu programu bure kwa siku 7
Anza bure

PixelPOS + Mashine ya POS

Skrini maalum ya kaunta

TZS 550,000
mwaka wa kwanza, pamoja na vifaa
Kisha TZS 250,000 kwa mwaka
  • PixelPOS kwa miezi 12: mauzo, stoo, madeni, ripoti
  • Mashine ya POS
  • Jaribu programu bure kwa siku 7
Chagua kifurushi hiki

Kaunta kamili

Mashine, droo ya pesa na printa ya risiti

TZS 750,000
mwaka wa kwanza, pamoja na vifaa
Kisha TZS 250,000 kwa mwaka
  • PixelPOS kwa miezi 12: mauzo, stoo, madeni, ripoti
  • Mashine ya POS
  • Droo ya pesa
  • Printa ya risiti
  • Jaribu programu bure kwa siku 7
Chagua kifurushi hiki
Vifaa vinaletwa baada ya malipo. Lipa kwa M-Pesa. Uliza kuhusu kufikishiwa mkoa wako
Android na iPhone

Duka lako, mfukoni mwako

Programu ya PixelPOS ina duka, stoo na madeni yaleyale ya kompyuta. Uza, angalia kilichobaki na uone faida ya leo ukiwa popote.

Inakuja karibuniGoogle Play Inakuja karibuniApp Store

Programu inakuja kwenye maduka ya programu. Kwa sasa, duka lako linafanya kazi kwenye kivinjari cha simu yoyote, kama skrini hii.

PixelPOS ikiwa wazi kwenye simu

Fungua duka lako kwa hatua tatu

01

Jisajili

Chagua jina na anwani kama dukalako.pixelpos.co.tz.

02

Weka bidhaa zako

Bei ya kununua, bei ya kuuza na idadi uliyonayo. Au ziingize kutoka Excel.

03

Anza kuuza

Duka lako linakuwa tayari kwa dakika mbili hivi, na wiki ya kwanza ni bure.

Maswali

Wanachouliza wenye maduka kwanza

Nini kinafuata baada ya wiki ya bure?

Taarifa zako zote zinabaki. Lipa TZS 250,000 kwa mwaka kupitia M-Pesa uendelee kuuza. Hakuna makato ya moja kwa moja.

Ni lazima ninunue vifaa?

Hapana. PixelPOS inafanya kazi kwenye simu, tablet au kompyuta uliyonayo. Mashine ya POS, droo ya pesa na printa ya risiti ni kwa maduka yanayotaka kaunta kamili.

Mwaka wa pili unagharimu kiasi gani?

TZS 250,000 kwa mwaka, kifurushi chochote ulichochagua. Vifaa vinalipwa mara moja tu.

Naweza kuandika madeni?

Ndiyo. Andika madeni ya kupokea na ya kulipa, pokea malipo kidogo kidogo, weka tarehe ya kulipa na uone yaliyochelewa. Mkumbushe mteja kwa WhatsApp moja kwa moja.

Wafanyakazi wanaweza kuwa na akaunti zao?

Ndiyo. Kila mfanyakazi anaingia kwa akaunti yake, na wewe unaamua anachoweza kuona na kufanya.

Taarifa za duka langu ni siri?

Kila duka lina database yake binafsi, iliyotengwa na maduka mengine na yenye nakala. Wanaoiona ni wale tu uliowapa akaunti.

Fungua duka lako leo

Siku 7 za kwanza ni bure. Hakuna kadi.