Sera ya faragha
PixelPOS ni mfumo wa mauzo kwa maduka. Mmiliki wa duka hufungua duka kwenye pixelpos.co.tz, na yeye pamoja na wafanyakazi wake hutumia tovuti au programu ya simu ya PixelPOS kurekodi mauzo, stoo, wateja, madeni na matumizi. Ukurasa huu unaeleza tunachohifadhi, kwa nini, na jinsi ya kukifuta.
Tunachohifadhi
- Taarifa za akaunti: jina, barua pepe na namba ya simu ya mmiliki wa duka na ya kila mfanyakazi anayesajiliwa, pamoja na nenosiri lililofichwa (hashed).
- Kumbukumbu za duka zinazoingizwa na duka lenyewe: bidhaa, bei, stoo, mauzo na risiti, manunuzi, matumizi, madeni, na majina na namba za simu za wateja na wasambazaji wa duka.
- Anwani ya arifa kwa kila simu inayoruhusu arifa: tokeni kutoka Google Firebase Cloud Messaging, inayotumika tu kuitumia simu hiyo arifa za duka (kwa mfano muhtasari wa asubuhi). Hufutwa unapotoka kwenye programu.
- Kumbukumbu za kuingia: muda, aina ya kifaa na anwani ya IP ya kila kuingia, ili mmiliki aone duka limeingia wapi na aweze kuondoa kifaa.
- Kumbukumbu za usajili na malipo ya kifurushi cha PixelPOS cha duka. Taarifa za kadi au pesa za simu hushughulikiwa na mtoa huduma wa malipo, hazihifadhiwi kwetu.
Tusichofanya
- Hatuuzi wala kushirikisha taarifa za duka kwa watangazaji. Programu haina matangazo.
- Hatusomi mawasiliano yako, ujumbe, picha wala mahali ulipo. Kamera hutumika tu unapochagua kuskani barcode au kuweka picha ya bidhaa.
- Vikumbusho vya SMS au WhatsApp kwa mteja hutumwa tu pale mfanyakazi wa duka anapochagua kutuma.
Nani anaweza kuona
Kila duka lina hifadhidata yake tofauti. Ni akaunti zilizosajiliwa na mmiliki pekee zinazoweza kuingia kwenye duka hilo, na mmiliki huamua kila akaunti inaona nini. Wafanyakazi wa PixelLinx huingia kwenye taarifa za duka tu kulisaidia duka kwa ombi lake au kuendesha huduma. Taarifa huhifadhiwa kwenye seva zetu na husafirishwa zikiwa zimefichwa (HTTPS).
Tunahifadhi kwa muda gani
Kwa muda wote duka linapotumika. Duka linapofunga akaunti, hifadhidata yake hufutwa ndani ya siku 30. Kumbukumbu za malipo huhifadhiwa kwa muda unaotakiwa na sheria.
Kufuta akaunti au taarifa zako
Akaunti ya mfanyakazi huondolewa na mmiliki wa duka chini ya Usimamizi wa Watumiaji. Mmiliki anayetaka duka lote na taarifa zake zifutwe, au mteja wa duka anayetaka taarifa zake ziondolewe, anaweza kutuandikia kutoka barua pepe iliyo kwenye akaunti:
info@pixellinx.co.tz · 0676058891 (simu au WhatsApp)
Tuambie anwani ya duka (kwa mfano myshop.pixelpos.co.tz). Tunathibitisha ombi na mmiliki, tunafuta taarifa ndani ya siku 30, na tunakujibu ikikamilika.
Mawasiliano
PixelLinx Technologies, Dar es Salaam, Tanzania. info@pixellinx.co.tz